October 2, 2018


Baada ya kuzidiwa kwa kila kitu Jumapili ya wiki jana na watani zao wa Simba katika mechi ya watani wa jadi, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amekiri kuwa walipata wakati mgumu mno.

Zahera ambaye alieleza mara baada ya mechi kuwa waliwaaachia Simba kuucheza mpira walivyotaka, leo ameibuka kivingine na kusema hakika walizidiwa kila idara.

Kocha huyo Mkongomani, ambaye alitua Yanga kuchukua mikoba ya Mzambia, George Lwandamina, amekiri kuzidiwa kwenye kipute hicho akieleza kuwa Simba walikuwa na uwezo mkubwa kuliko wao.

Aidha, licha ya kuwataja viungo wake Dues Kaseka na Ibrahim Ajibu kuwa walikuwa sababu ya Yanga kushindwa kuhimili mikiki ya Simba, Zahera amewaongeza wengine kwa orodha ambao walisababisha Yanga kupigwa kete na Simba.

Wachezaji aliowaongeza ni kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' pamoja na Papy Kabamba Tshishimbi kuwa sehemu ya wachezaji ambao hawakufuata maelekezo aliyowapa na kuepelekea kuzidiwa na watani zao.

5 COMMENTS:

  1. Yanga tulilala na viatu. Kwa mara ya kwanza niliomba mpira uishe.Tatizo baada ya kukubali ukweli kwamba standard yetu ya mpira kwa sasa ipo chini kulinganishs na Simba.Inauma lakini ndio ukweli.Tutafute njia ya kupandisha kiwango cha timu yetu.

    ReplyDelete
  2. Bado huo ni mwanzo tu kwani kwa jinsi Simba hata macho yanampongeza mtazamaji kwa kuyatuma kwa kutizama kinachostahili kutizamwa. Hongereni Simba ila msivimbe kichwa tafuteni dawa ya washambiaji wengi kwani hakuna alie nashaka na uwezo wao lazima kuna kitu.

    ReplyDelete
  3. sidhani kama ni maoni ya kiungwana kutolewa na KOCHA.

    ReplyDelete
  4. Kocha kasema kweli. Inabidi utamaduni wa kusema kweli uendelezwe kwenye hizi timu mbili. Pongezi kwa Simba kwa kucheza mpira wa kuigwa .Mimi ni Yanga lakini nimeamua kusema ukweli .

    ReplyDelete
  5. Shida sio kuzidiwa na simba tu hats stand walitusumbua Sana kuna vitu lazima wachezaji wakubali na wabafilike ili timu iwe bora

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic