October 2, 2018


Mlinda mlango wa klabu ya Yanga, Beno Kakolanya, amemtaja kiungo wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, kuwa ndiye aliyesababisha kupata changamoto kubwa langoni kwake.

Kakolanya ameamua kufunguka juu ya mchezaji huyo kwa kumuelezea kuwa alileta wakati mgumu langoni kwake jambo lilimfanya kupambana kwa juhudi zote ili kuepusha msala.

Kipa huyo ambaye alikuwa hachezi mara zote wakati Mcameroon Youthe Rostand akiwa ndani ya timu hiyo, amesema kila mpira ulipokuwa unaguswa na Chama lazima ulete madhara.

Ameeleza kuwa Chama alikuwa akijitahidi kuwapikia vizuri wenzake jambo ambalo lilipelekea kutengeza nafasi nzuri kwa Simba na yeye akawa anapambana kuepusha shari kwa kucheza mipira ya washambuliaji hatari wa Simba.

"Alikuwa mwiba kwetu, yeye ndiye aliucheza mwingi na kuutawanya, lakini tunashukuru kwa kufanikiwa kutoka sare na sasa tunaangalia mechi zingine" alisema.


Baada ya mechi hiyo, tayari Simba na Yanga zimeshaanza maandalizi kuelekea mechi zijazo za ligi ambapo Simba atacheza na African Lyon huku Yanga akicheza na Mbao FC.

1 COMMENTS:

  1. Chama ni level nyingine kulinganisha na wachezaji wetu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic