November 21, 2018


Nyota wa timu ya Yanga, Ibrahimu Ajibu amesema kuwa ataendeleza rekodi yake ya kufanya maajabu awapo uwanjani kwa kuwa muda wa kuisaidia timu ni sasa.

Ajibu amefanikiwa kuhusika katika mabao 12 kati ya 17 ambayo Yanga wamefunga kwenye michezo 10 waliyocheza.


"Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha matokeo yanapatikana, kila nikipata nafasi ni lazima niitumie ipasavyo kwani nafanya kazi kwa ajili ya timu yangu.


"Ushirikiano uliopo ndani ya timu unatujenga na kufanya tuwe katika hali ya furaha muda wote, hivyo tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo," alisema.


Mwadui FC wataikaribisha Yanga kesho kwenye uwanja wa Kambarage huku rekodi zikionyesha kuwa Yanga hajapoteza mchezo hata mmoja kati ya 10 aliyocheza huku Mwadui FC akiwa amepoteza michezo 6 kati ya 13 aliyocheza.

2 COMMENTS:

  1. kivipi awaumize simba jamani unamaana kagere na okwi wanaumiza yanga sio

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic