November 21, 2018


Na George Mganga

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia, amewataka mashabiki na wadau wa mpira wa miguu nchini kuacha kuingilia majukumu ya Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike.

Karia amevunja ukimya kwa kusema Amunike anapaswa kuheshimiwa juu ya taaluma yake hivyo ni vema akaachwa ili atimize wajibu wake.

Hayo yamekuja kufuatia Kocha Amunike kuanza kutupiwa vijembe na hata lugha isiyo rafiki baada ya Taifa Stars kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019 huko Cameroon.

Rais amefunguka hayo kutokana na Amunike kushutumiwa jambo ambalo anaamini ni kuingiliwa kwa taaluma ya kocha huyo ambaye aliwahi kusakata kambumbu la kimataifa.

Sanjari na hayo, Amunike amewataka mashabiki wa soka nchini kuwa na uvumulivu kwani Stars itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Uganda ambao ana imani timu itafanya maajabu na kufuzu.


13 COMMENTS:

  1. Uongozi ni pamoja na kupokea lawama pale matokeo yasipowaridhisha wadau, sasa hofu ya nini? Mbona wachezaji mnafika pahali mnawatema na kusema viwango vyao haviridhishi? Hakuna ubaya kumkosoa kocha. Mbaya kama itatumika lugha ya matusi, hiyo hapana. Lakini kumkosoa ni jambo zuri. Hawezi kukwepa kukosolewa hii ni timu ya Taifa, ni ya wananchi wote.

    ReplyDelete
  2. Kwani Amunike na mzee Wenger aliekuwa kocha wa Arsenal nani anataaluma zaidi ya ukocha? Huyu raisi wa TFF vipi lakini? Huu udikteta wake wa kutosikiliza na kutokujali mawazo ya watu wengine ndio chanzo cha uozo wote unaoziandama timu zetu za taifa. Kuna wanataaluma wangapi walioheshimiwa na mwisho wa siku wakasababisha maafa.Wadau mapema tu walijua Amunike sio kocha alietayari kwa kazi aliekabidhiwa lakini wakaoneakana maadui sasa ukweli unadhihiri waliomleta wanawatisha watu mitaanai kutosema chochote? Watanzania wapo huru kutoa maoni yao tena sio vizuri kabisa kusikia kauli za kibabe kama hizi kutoka kwa kiongozi wa juu anaesimamia taasisi ya michezo ya wananchi. Vipi watanzania wakiamaua kuisusia timu ya Taifa? Kwakuwa wanaona maoni yao yanapuuzwa na si kupuuzwa tu bali wanatishwa yeye Karia atajisikiaje?

    ReplyDelete
  3. Karia na Amunike wako tutawasuia timu yenu hatutaki ujinga

    ReplyDelete
  4. Huyu Karia anaonyesha amefeli kabisa kuliongoza shirikisho hana watu sahihi Wa kumsaidia kutafuta makocha Wa timu za Taifa. Taifa stars imetuzingua, Kilimanjaro warriors nayo imetolewa na Burundi. Kwakifupi chini ya karia kila michuano tunayogusa tunapigwa tu!

    ReplyDelete
  5. Karia si mtu wa mpira hate kidogo. Malinzi alikuwa na mapungufu yake lakn aliamua kukipandisha hadhi kikosi cha Serengeti kuwa Ngorongoro...kutengeneza Stars maboresho na vingne. Karia kaja kafuta huo mpango. Ile timu ndogo ya Serengeti ilipandishwa hadhi Sasa imetupwa wamepandishwa vijeba. Angalia Jana...ile ndio ilitakiwa kucheza Ngorongoro ya kina Nashon..Kibabage na Yohana Mkomola. Tumeletewa wachezaji wengine.
    Muulize Amunike mwenyewe kama ni kwel kikosi Chao kilikuwa kinabomolewa kila mara..timu ilikuwa na mabeki 7...hakukuwa na midfield mbunifu wote walikuwa wavunja mbao. Sasa kama unajilinda zidi ya Lesotho je tukicheza na Cameroon si ndio tutaamua kuja kulala golini kabisa.
    Tuongee ukwel kocha na washauri wake wametuangusha sana..wametufanya tuanze na mpango wa kubahatisha wakati tayar hesabu zilikuwa nzur. Mi niliamini kikosi kilichocheza na Cape Verde kingebaki na kujaribu kumtafuta mbadala wa Mbwana na si kukibomoa kabisa. Ila sisi tulikibomoa aisee. Tunashukuru kwa maamuzi mliyotupa.
    Ila tunaendelea kuwaombea Mungu wachezaji waje wafanye vizur kwenye mechi ijayo na si kea faida ya TFF ila ni kwa faida ya wachezaji wenyewe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wakifudhu sasa,, dhidi senegal wataingia walinzi 11 woote wanalala golin

      Delete
  6. Huyo Karia mcenge na hao wanaomsaidia na wanaomshauri Amunike ni wacenge vile vile. Lethoso? Lethoso wakutufirigisa sisi wanavyopenda? Ama kweli Aaa!

    ReplyDelete
  7. Unavyomwongelea amunike na kaliaa woteee sawaa tuu...kalia hamana chochote tena akae kimyaa asiamshe hasira zetuu

    ReplyDelete
  8. Hongera Karia.Smjlike ni binge LA Kocha.msimpoteze.Mpira Wa Tz hapo ndipo unapo haribikia.Mashabiki kumpa covha mchezaji wao aitwe time ya taiga na pia hats list ya kucheza ipangwe na wao.
    Tatizo hapa unapambana na bifu kati us simba na Amulike,sio matokeo ya Lesotho.Amuloke hakumpanga Mkude,hii ndio taabu.lakinini Kama ulivyosema wamwachie mwenye taaluma take abadilishe Moira Wa Tz.kocha anayeletwa na magazeti atakuja kutolewa na magazeti tu.akiletwa na mashabiki atatolewa na mashabiki.watu wajifunze kuheshimu taaluma na tff

    ReplyDelete
  9. rais wa TFF umekosea, kumbuka mashabiki wa soka hapa nchini ,ni watanzania na hiyo ni timu yetu tunapaswa kuhoji ,kama kuna ubovu tusihoji , kocha kama anaboronga tukae kimya inasaidia nini ,ili iweje , tutaendelea kupiga kelele mbaka tuone mabadiliko katika hii timu, mtu anaharibu timu ya taifa halafu unasema tukae kimya , haiwezekani ukweli utasemwa,aibu hii haifai kwa taifa kama hili ,msitengeneze uoga kwa raia. watu tunapaswa kuhoji , kocha hafai

    ReplyDelete
  10. Taifa Stars haitaweza kuifunga Uganda Cranes

    ReplyDelete
  11. Ukiona mtu anapewa maoni/ushauri anapandisha hasira na vitisho ujue kichwa maji anaamua kujihami. Karia anafikiri akikubali kukosolewa basi ameshindwa kumbe ndiyo njia ya kujiimarisha. Amka karia

    ReplyDelete
  12. Nimeamini tanzania WANAOSHINDA NI C.C.M tu. Hakna cha serengeti boys, wala ngorongoro wala taifa star, wakitaka kushinda SHETAN anakja anaharibu, kwa sahiz AMUNIKE hajui tuwe wakwel hata MORINHO anadefence lakn sio kwa kutumia walinzi 9 na straiker 2
    MFANO: stars wangetoa sare kwa akina cape vede ingesaidia na lesoto tutoe sale ama tushinde hal ingekuwa nzr lakn SHETAN akamtumia AMUNIKE

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic