November 10, 2018


Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Abdulhalim Humud, ameamua kuondoka Dar es Salaam na kwenda kujiongezea dozi ya mazoezi mkoani Tanga ili kulinda kipaji chake.

KMC walimpa ruhusa Humud kuwa mchezaji huru baada ya yeye mwenyewe kuomba kutokana na kile kilichoelezwa ni utovu wa nidhamu alioufanya ndani ya klabu ikiwa ni pamoja na kusahau vifaa vya michezo Dar es Salaam wakati timu ilipocheza na Coastal Union na kuwasumbua wake wa wachezaji wenzake.

"Nimeondoka Dar kwa sasa nipo Tanga ambapo naendelea na mipango mingine, kwa sasa nafanya sana mazoezi ili kujiweka fiti zaidi, kuhusu masuala ya kwenda mahakamani hilo nawaachia viongozi wangu.

"Sina kinyongo na KMC ninachotaka ni amani ya moyo wangu na kufanya kile ambacho ni sahihi, siwezi kuwa mnafiki siku zote nitasimamia kweli kwa kuwa najiamini na nina kipaji," alisema.


KMC kupitia Ofisa habari, Anwar Binde, umesema kuwa Humud anapaswa atambue kuwa KMC ni taasisi kubwa ambayo inafuata misingi yote ya kazi na kusimamia haki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic