November 10, 2018



Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Malangwe Mchungahela amewaonya wanachama wa Yanga ambao wanaopinga uchaguzi wa Yanga uliopangwa kufanyika baada ya viongozi wao kujiuzulu.

Mchungahela amewataka wanachama kuwa watulivu na kuunga mkono juhudi za kutaka kupata viongozi wapya kwa maendeleo ya klabu na sio kuleta malumbano ambayo hayana faida.

"Tuna taarifa kwamba kuna baadhi ya viongozi wa Yanga wa kamati ya utendaji na baadhi ya wanachama wanataka kuvuruga mchakato wa uchaguzi na kesho jumapili wanataka kuitisha kikao chao cha kumtambua mwenyekiti Yusuphu Manji.

"Nataka tu kuwaonya wasithubutu kufanya hivyo na wakifanya tutawashughulikia hatutawachekea, mchakato umeshatangazwa nafasi ya mwenyekiti ipo wazi imetangazwa, anayetaka uenyekiti aje achukue fomu, hivyo wasipite mlango wa nyuma," alisema.

Kamati ya Utendaji ya Yanga jana ilimtangaza Thobias Lingalangala kuwa kaimu mwenyekiti wa Yanga baada ya Manji kuamua kujiuzulu tangu Mei mwaka jana na wapo kwenye mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Januari 13, mwaka huu.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic