November 11, 2018


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema malengo yake kwa sasa ni kuhakikisha anawashusha Azam kwenye nafasi ya kwanza.

Aussems ameeleza sasa hivi mikakati aliyonayo na kuiwezesha Simba kukaa kileleni bila kushuka kwenye nafasi hiyo tayari kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu.

Kocha huyo anaimani ligi ina ushindani mkubwa na changamoto zake lakini atapambana kwa namna yoyote ile kuchukua nafasi hiyo.

Mbelgiji ameeleza pia anatambua kuwa Yanga wana mchezo mmoja mkononi lakini hilo halimpi tabu kwa sababu malengo yake ni kupanda mpaka nafasi ya kwanza.

Msimamo huo unaonesha Azam FC ipo kileleni ikiwa na alama Azam 30 huku ikifuatia Simba iliyo na 26 pamoja na Yanga yenye 26.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic