November 24, 2018


Na George Mganga

Kocha Msaidizi wa Lipuli FC, Seleman Matola, amesema matokeo waliyoyapata jana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, yaliyotokana na mbinu ambazo waliziandaa dhidi ya mabingwa hao watetezi wa ligi.

Akizungumza mara baada ya mchezo, Matola ameeleza kuwa waliingia na mbinu tofauti ambazo ziliwafanya Simba washindwe kucheka na nyvavu na kusababisha mchezo kumaliza kwa suluhu tasa ya 0-0.

Aliongeza kuwa licha ya kuwabana Simba kikosi chake pia kilikosa nafasi kadhaa ambazo ama wangeweza kuzitumia vema wangeweza kuondoka na alama zote tatu dhidi ya Simba.

"Mbinu ambazo tuliingia nazo zilitusaidia kupata matokeo ya aina ile japo tulipata nafasi nyingi za kufunga lakini washambuliaji wangu hawakuwa vizuri" alisema.

Katika mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ulishudiwa Simba wakitawala mechi kwa asilimia kubwa huku washambuliaji wake wakiongozwa na Meddy Kagere pamoja na John Bocco wakishindwa kucheka na nyavu.

Aidha, Matola amezungumzia juu ya tetesi ambazo zimeenea kuwa anahusishwa kutua Simba ili kuchukua nafasi ya aliyekuwa Koch Msaidizi, Masoud Djuma, kuwa si za kweli bali ni mitandao imekuwa ikiandika.

"Si kweli, ni watu tu wamekuwa wakiandika mitandaoni wala Simba wenyewe hawajawahi hata kunipigia simu kama wananihitaji" alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic