Beki huyo ambaye ndiye nahodha wa Rayon amekiri kufanya mazungumzo na Simba na kusema kuwa wamekuja na ofa nzuri kuliko ile ya Yanga.
Mchezaji ameeleza kuwa Simba wamekuja na ofa nzuri ambayo hata mshahara wake utakuwa mkubwa tofauti na ile ya Yanga waliyoileta mezani.
Rwatubyaye amekuwa mmoja wa wachezaji tegemeo Rayon na inaelezwa dau limepanda la kumg'oa ili kumtoa ndani ya klabu yake kwenda Simba tofauti na ilivyokuwa kwa Yanga.
Dirisha la usajili wa wachezaji wa mpira wa miguu hapa nchini litafunguliwa Novemba 15 2018 ambapo tayari kila timu imeshaanza harakati zake ili kuongeza nguvu kwenye vikosi.
simba tuwachieni nao watasema tunawanyanyasa maana kila mchezaji akitakiwa na yanga tunawapokonya kisa pesa.
ReplyDeleteHuyu atachukua nafasi ya Juuko kama atafanikiwa kujiunga na Orlando pirates
Delete