November 30, 2018


Beki wa kulia wa Simba, Zana Coulibaly ambaye amesaini leo kandarasi ya miaka miwili na kupewa jezi namba 21 amesema kuwa amekuwa akiwasikia wapinzani wa timu yake Yanga hivyo anajipanga kuweza kuonesha maajabu.

Beki huyo ambaye amesajiliwa ili kuziba nafasi ya beki Shomari Kapombe ambaye amefanyiwa operesheni ya enka ya mguu baada ya kupata majeruha alipokuwa na timu ya Taifa ilipokuwa kambini nchini Afrika kusini, leo ameanza mazoezi na kuonyesha kasi akiwa uwanjani.

"Ninaamini Yanga ni timu bora yenye wachezaji wazuri na kazi kubwa itakuwepo mara nitakapokutana nao, mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na upinzani uliopo," alisema.

Coulibaly ni raia wa Burkina Faso ametokea klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast alishuhudia Simba wakitakata mbele ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili kwa kupata ushindi wa mabao 4-1, ana umri wa miaka 26.


2 COMMENTS:

  1. Waandishi wa bongo bwana, Yan swali lenu la Kwanza ni yanga hahahaha waandishi uchwara

    ReplyDelete
  2. Yeye ndo kafika kajuaje kama wapinzani wa Simba ni Yanga? Kuna timu nyingi zaidi ya Yanga ambazo zinacheza mpira mzuri kupita timu hiyo. Andikeni habari msiandike mawazo yenu

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic