November 28, 2018

Mshambuliaji wa timu ya Simba, John Bocco anawanyanyua mashabiki wa Simba kwa kufanikiwa kumrudisha kwenye nyavu mara mbili mlinda mlango wa Mbabane Swallows ya Swaziland.

Bocco amefanikiwa kufanya hivyo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unachezwa uwanja wa taifa baada ya kufunga mabao 2.


Bao la kwanza Bocco alifunga akimalizia pasi iliyopigwa na Nicolas Gyan dakika ya 7 na bao la pili akafunga kwa penati baada ya mlinda mlango wa Mbabane kumchezea rafu Emanuel Okwi.


Mbabane wamefunga bao 1 dakika ya 24 lililofungwa nje ya 18 na Guevane Nzambe, na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa Simba 2-1 Mbabane.


Kipindi cha pili Meddie Kagere alifunga bao la 3 dakika ya 83 akitumia vema makosa ya mlinda mlango wa Mbabane na bao la 4 likifungwa na Claytous Chama akimalizia pasi mpenyezo ya Hassan Dilunga dakika ya 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic