November 29, 2018


Uongozi wa Coastal Union umemtumia salamu za heri ya kuzaliwa mchezaji wao Alli Kiba ambaye ni mdhamini wa timu hiyo pamoja na mwanamuziki wa kizazi kipya.

Kocha Mkuu, Juma Mgunda amesema kuwa wanatambua thamani ya Kiba ndani ya timu na mahitaji ya mashabiki kumuona uwanjani hivyo atarejea uwanjani baada ya kumaliza ratiba zake.

"Wengi wanamtambua Kiba, ila mimi natambua uwezo wake na umuhimu wake ndani ya kikosi, atarejea rasmi kwenye timu na ataonekana akifanya kazi yake uwanjani.

"Baada ya kumaliza kazi zake sasa ataripoti kambini Desemba 1 na ataanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kuendeleza moto wake kwenye Ligi kuu," alisema.

Coastal Union wamecheza michezo 114 na kujikusanyia pointi 22 wakiwa nafasi ya 5 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

2 COMMENTS:

  1. Kila nkisoma habar zako zimejaa makosa kibao kma vipi kaaa pembeni
    Coast union wamechez match 114!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic