November 30, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema wachezaji wake wamechza mchezo wa jana dhidi ya JKT Tanzania bila kula chakula cha mchana.

Zahera ameeleza kwamba wachezaji wake walikosa chakula kutokana na mabadiliko ya muda wa mchezo yaliyofanywa na Bodi ya Ligi kutoka Saa 12 kama ilivyokuwa awali kwenda Saa 10.

Kocha huyo ameoneshwa kushangazwa na maamuzi hayo ya bodi ya ligi kufanya hivyo wakati ilikuwa inajulikana mchezo utapigwa majira ya saa 12 za jioni.

Kupitia Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo, aliibuka na kusema mechi zote ambazo zilikuwa zinachezwa saa 12 na saa 1 usiku kwa Dar es Salaam, sasa hivi zitachezwa saa 10 kama ilivyokuwa mwanzo.

Ndimbo amesema mabadiliko hayo yamekuja baada ya serikali kuzuia ili kuepusha matumizi ya taa kwa usiku na sasa zitaendelea kupigwa saa 10.

Katika mchezo wa jana uliopigwa uwanjani hapo, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania.

1 COMMENTS:

  1. Kwani mkisema tu ukweli kuna shida gani! Hela ya kula mlitrgemea baada ya mapato ya mlangoni! Njaa mbaya!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic