November 8, 2018


Antonio Conte amekataa mkutano na Chelsea na anasisitiza kuhusu kuwapeleka mahakamani kwa mshahara wake uliosalia, baada ya kufutwa mwezi Julai huku mwaka mmoja ukisalia kabala ya kukamilika mkataba wake. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Tottenham Fernando Llorente, 33, amasema atatumia fursa kurejea Uhispania baada ya kuwa na wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza huko Tottenham. (London Evening Standard)

Manchester United wanataka kumsaini mchezaji wa Sampdoria mwenye miaka 22 mlinzi raia wa Denmark Joachim Andersen. (La Republica, via Mirror)

Mexico wanafakiria kumteua meneja wa zamani wa Watford Quique Sanchez Flores kuwa meneja wao. (ESPN - in Spanish)

Southampton wanandaa pauni milioni 15 za kumsaini mshambuliaji wa Portimonense raia wa Japan Shoya Nakajima, 24. (Record, via Talksport)

Wing'a wa Lille Nicolas Pepe, 23, amekaribisha uvumi unaomhusisha na Arsenal na vilabu vingine vinavyoongoza Ulaya lakini anasisitiza kuwa ni mapema sana kupangia msimu ujao. (London Evening Standard)

Rais wa Fifa Gianni Infantino anasema kombe la dunia la mwaka 2022 nchini Qatar pia litaandaliwa na nchi majirani zake. (Times - subscription required)

Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic, 37, anasema hawezi kuhamia klabu ya Ulaya kwa mkopo wakati huu msimu wake huko MLS umekamilika. (Mirror)

Mlinzi wa zamani wa Tottenham Paul Miller ambaye sasa ni baloziwa klabu, anaamini kujengwa uwanja wa White Hart hakuwezi kukamilika kuandaa mechi za kwanza za timu hadi Februari. (Love Sport Radio)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Manchester City, Bolton na Chelsea Nicolas Anelka amekuwa kwenye mazungumzo na Lille kuhusu kuwa kocha wa timu yao ya vijana kwenye klabu hiyo ya Ufaransa. (L'Equipe - in French)


Brighton wanajadili kuhusu ikiwa watamtoa kwa mkopo mchezaji wao mwenye miaka 18 Aaron Connolly mwezi Januari au kumpeleka kwenye klabu ya wachezaji walio chini ya miaka 23. (Argus)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic