November 30, 2018


Mlinda lango wa Manchester United David de Gea, 28, anasubiri kuona iwapo Jose Mourinho atakuwa bado ndiye meneja wa klabu hiyo msimu ujao kabla ya kukubali kutia saini mkataba mpya katika klabu hiyo. (Mirror)

Juventus wataanza kumuangazia kiungo wa kati Paris St-Germain na Ufaransa Adrien Rabiot, 23, iwapo mchezaji wa Arsenal raia wa Wales Aaron Ramsey, 27, atakataa kujiunga na klabu hiyo ya Serie A. (Sun)

West Ham watampa nyota wa zamani wa Arsenal na Manchester City Samir Nasri mkataba mpya wa miezi sita iwapo atathibitisha kwamba yuko sawa kucheza. Mchezaji huyo mwenye miaka 31 amekuwa akifanya mazoezi na West Ham anapojiandaa kukamilisa marufuku ya kutumia dawa zisizoruhusiwa michezo, marufuku inayodumu hadi siku ya Mwaka Mpya. (Mirror)

Kinda wa Manchester City na Uhispania Brahim Diaz, 19, amefikia makubaliano yasito rasmi ya kujiunga na miamba wa Uhispania Real Madrid mwezi Januari. (Goal)

Mkurugenzi wa uchezaji wa zamani wa AC Milan Massimiliano Mirabelli anasema klabu hiyo ilijaribu kumnunua nyota wa Ureno anayechezea Juventus kwa sasa Cristiano Ronaldo, 33, majiraya joto yaliyopita, lakini wamiliki wa wakati huo wa AC Milan walipinga mpango huo. (Sportitalia kupitia Mail)

AC Milan wameanza mazungumzo ya kutaka kumchukua kiungo wa kati wa Uhispania na Chelsea Cesc Fabregas, 31. (Calciomercato)

Manchester City wana nafasi nzuri sana ya kumnunua kinda wa Benfica kutoka Ureno mwenye miaka 17 Tiago Dantas. (Record, kupitia Manchester Evening News)

Arsenal na Tottenham wanaongoza katika mbio za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Ujerumani anayechezea Hoffenheim Nadiem Amiri, licha ya kwamba mchezaji huyo mwenye miaka 22 hajacheza mechi hata moja msimu huu kutokana na majeraha. (Bild kupitia Sun)

Cesc Fabregas amekuwa hachezeshwi sana Chelsea msimu huu
Watford wanamfuatilia kwa karibu winga wa England anayechezea Nottingham Forest Joe Lolley, 26. (Mail)

Meneja wa Burnley Sean Dyche amewatahadharisha mashabiki wa klabu hiyo wasitarajie 'mafuriko' ya wachezaji wapya kwenye klabu hiyo soko litakapokuwa wazi Januari licha ya kuteuliwa kwa Mike Rigg kuwa mkurugenzi wa kiufundi. (Lancashire Telegraph)

Meneja wa Aston Villa Dean Smith atafanya uamuzi kuhusu mchezaji James Collins ambaye amekuwa akifanyiwa majaribio katika klabu hiyo muda si mrefu. Beki huyo mwenye miaka 35 amekuwa bila klabu tangu kuihama West Ham majira ya joto na amekuwa akifanya mazoezi na Aston Villa. (Birmingham Mail)

Meneja wa Celtic Brendan Rodgers amesema beki wa Leicester Filip Benkovic, 21, ambaye yuko katika klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mmoja ni mchezaji stadi sana na kwamba yuko tayari kucheza Ligi ya Premia. (Daily Record, kupitia Leicester Mercury)

Arsenal wanatafakari uwezekano wa kuwafidia mashabiki takriban 800 waliokuwa wamenunua tiketi za kutazama mechi ya Europa League dhidi ya Vorskla ambayo ilihamishiwa Kiev kutokana na sababu za kiusalama Ukraine. (London Evening Standard)

Kwa mujibu wa BBC

FANYA KUMFOLLOW SALEH JEMBE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

INSTAGRAM ===>SALEHJEMBE

TWITTER ===> SALEH JEMBE

FACEBOOK  ===> SALEH JEMBE

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic