Mchezaji kinda wa AC Milan, Raoul Bellanova amezua gumzo baada ya kupiga picha na Cristiano Ronaldo baada ya mechi yao dhidi ya Juventus kutokana na nahodha wa Juve, Giorgio Chiellini kuonekana akiwa mtupu kabisa.
Bellanova aliingia kpiga picha na Ronaldo mara baada ya mchezo kati ya timu hizo mbili kumalizika.
Licha ya kuwa ugenini, Juventus waliibuka na ushindi huku Cristiano Ronaldo akiibuka mmoja wa mashujaa akifunga bao moja sawa na Mario Mandzugik.
Wengi wamekuwa wakijadili namna ambavyo picha hiyo haikupaswa kutumika mitandaoni.
Wanaamini Bellanova angeweza kumficha Chiellini kwa kuwa naye hakujua wakati picha hiyo ikipigwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment