November 9, 2018


Rekodi bado zinaendelea kuandikwa kwenye ligi ya msimu huu ambapo baada ya Meddie Kagere kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao la mapema dakika ya pili kisha Mrisho Ngassa dakika ya kwanza mchezaji wa Mtibwa Sugar, Kelvin Sabato amewafunika wote.

Sabato alifanya hivyo katika mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro baada ya kufunga bao la kwanza ndani ya sekunde 53. 

Kwa mujibu wa Spoti Xtra, Sabato alisema; “Kila mchezaji nia yake ni kuona timu inafanikiwa kupata matokeo hivyo nitaendelea kufanya hivyo kila ninapopata nafasi kwenye timu yangu.”

“Ushindani ni mkubwa na ndio maana ukiangalia zimepita mechi nyingi mpaka kufanya hivyo nina imani kuna mengi ambayo yatatokea msimu huu kutokana na ushindani uliopo hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” alisema Sabato.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kuwa bao la mapema la Sabato lilisaidia kuivuruga Ruvu Shooting ya Masau Bwire na kufanikisha kuongeza mengine matatu kwa kuwa wachezaji walipaniki.


2 COMMENTS:

  1. Huko sawa kijana huu ni upumbavu,na sitaki kiwa mnafiki unadhidi kujiharibia credibility my brother.

    ReplyDelete
  2. Huna akili kabisa...yaani hapo sijaelewa ubabe ni upi?umekuwa unaandika upuuzi...sasa unaandika habari za chooni kabisa.Jua unachoandika kinatueleza kuhusu akili yako ilivyo na namna ya kuandika.Huna cha maana usiandike ...sio kutulisha hapa pumba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic