November 27, 2018


Uongozi wa klabu ya JKT Tanzania umeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwataka Yanga wasafiri kuelekea Mkwakwani, Tanga kwa ajili ya mechi dhidi yao ambapo watakuwa wenyeji.

Msemaji wa klabu hiyo, Jamila Mutabaza, ameeleza kuwa kwa sababu wao watakuwa nyumbani ni vema mechi hiyo ikapigiwa Mkwakwani.

Mubataza amesema kama Simba waliweza kusafiri na kwenda kukipiga Tanga basi ni vema pia Yanga wakaenda kwao kupigania alama hizo tatu.

Msemaji huyo ameeleza katika ligi huwa kuna mechi za nyumbani na ugenini hivyo wameitaka TFF mapema kuhakikisha wanawaambia Yanga waelekee Mkwakwani kwa mechi hiyo ya ugenini.

JKT Tanzania watakuwa wanacheza na Yanga Novemba 29 2018 na mara baada ya mechi hiyo itawabidi Yanga waelekee Mtwara raundi ya pili ya msimu kama TFF watakubali ombi la JKT.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic