November 27, 2018


Itakuwa mara ya kwanza kwa Ligi ya Mabingwa Afrika kuchezwa siku moja na ile ya Mabingwa Barani Ulaya maarufu kama UEFA Champions League, ambapo klabu ya Simba itakuwa inakipiga na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Ratiba ya CAF kwa sasa imepangwa kuchezwa siku moja na mechi za Ligi ya UEFA ili kuwapa burudani zaidi mashabiki wadau wa soka kwa ujumla Afrika na duniani kwa ujumla.

Wakati ratiba hiyo ikibadilishwa, vigogo kadhaa wa soka Ulaya ikiwemo Liverpool atakayekuwa ugenini dhidi ya PSG na FC. Barcelona dhidi ya PSV Eindhoven watakuwa wanashuka dimbani kesho.

Vigogo hao sasa wataungana na Simba ambayo inashiriki Ligi ya CAF Champions League kucheza siku moja ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu mabadiliko ya ratiba hiyo yafanyike.

Simba itakuwa mwenyeji kwenye Uwanja wa taifa, Dar es Salaam, mechi itaanza majira ya saa 10 kamili jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic