November 4, 2018


Mshambuliaji wa timu ya Simba, Meddie Kagere amefanikiwa kuwakosha viongozi pamoja na mashabiki kutokana na kufanikiwa kuipa pointi tatu timu ya Simba mbele ya JKT Tanzania na kuwashusha watani zao Yanga nafasi ya pili.

Kagere alifanikiwa kufunga mabao hayo katika mchezo wa jana uwanja wa Mkwakwani Tanga, ambapo Kocha Mkuu Patrick Aussems alisema kuwa uwanja haukuwa rafiki kwa timu ya Simba kutokana na kutokuwa na ubora.


Ofisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa mwendo ambao sasa Simba wamekuwa nao unawanyamazisha wapinzani wao kwa kuwa wanapata matokeo ambayo wanayahitaji.


"Tunajua kwamba tunatetea ubingwa na wachezaji wote tulionao ni bora hivyo tunafanya kazi tukiwa tunajiamini na mfumo ambao umeletwa na kocha tayari umejibu, tunapiga mpira na kushinda na kutoa burudani kwa mashabiki.


"Master Kagere kazima mdomo wa kocha wao, soka haichezwi mdomoni bali uwanjani na mchezji bora wa mwezi October ndiye aliyefunga mabao yote, mashabiki waendelee kutupa sapoti," alisema.


Ushindi huo unawafanya Simba wafikishe pointi 26 baada ya kucheza michezo 11 wakiwa nyuma ya Azam ambao wana pointi 27 baada ya kucheza michezo 11 na watani zao wanapointi 25 wakiwa nafasi ya tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic