November 11, 2018


Baada ya tetesi za muda mrefu na mvutano wa muda kuhusu usajili wake, hatimaye kiungo mchezeshaji wa Gor Mahia ya nchini Kenya, Francis Kahata, amefunguka juu ya taarifa za yeye kuwaniwa na Simba ya Tanzania.

Kahata hajataka kupindisha maneno, ameenda moja kwa moja kwenye pointi kwa kusema kuwa dili lake la usajili la kutua Simba likifanikiwa, basi msham­buliaji wa timu hiyo Mnyar­wanda, Meddie Kagere atapata nafasi ya kufunga kwa wingi.

Kahata ni kati ya wachezaji wanaotajwa kuwaniwa kwenye usajili wa dirisha dogo la Ligi Kuu Bara linalotarajiwa kufun­guliwa Alhamisi ijayo, Novemba 15.

Mkenya huyo katika usajili mkubwa uliopita, alikuwa ana­waniwa vikali pamoja na Kagere ambaye yeye usajili wake ulika­milika baada ya mkataba wake kumalizika Gor Mahia kabla ya kusaini Simba miaka miwili.

Kwa mujibu wa Championi Ijumaa, Kahata alisema hiyo kasi ya ufungaji mabao aliyo­nayo hivi sasa Kagere katika ligi siyo yake licha ya kusifiwa na mashabiki wa timu hiyo.

Kahata alisema mashabiki wa timu hiyo wakitaka kumfaidi mshambuliaji huyo, basi acheze naye timu moja kutokana na kumjulia aina yake ya uchezaji akiwa ndani na nje ya 18.

“Tukiwa hapa Gor Ma­hia, Kagere alikuwa ana­penda tucheze pamoja na alikuwa anafurahia tukianza wote kutokana na kumjulia mipira ipi nimpasie akiwa amefika kwenye hatari ya goli la wapinzani.

“Nikwambie huyo Kagere wanayemsifia watamuona mzuri zaidi kama mimi nikifani­kisha mipango yangu ya usajili ninayoendelea nao Simba, na nina matarajio makubwa ya kuja huko Simba.

“Hivi sasa ninasubiria ofa yao pekee lakini mipango mingine ya usajili in­akwenda vizuri, kama ikishindikana kuja Simba kutokana na Simba kushindwa kufi­kia muafaka mzuri na Gor Mahia,” alisema Kahata.

Kwa sasa katika ligi kuu anayeongoza kwa kufunga mabao ni Eliud Ambokile wa Mbeya City mwenye mabao 8 akifuatiwa na Kagere na Emmanuel Okwi wote wa Simba wakiwa na ma­bao saba kila mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic