November 11, 2018


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima amekiri kwamba kiungo mwenzake, Claytous Chama anaujua mpira vizuri lakini anamzidi uwanjani kwa sababu yeye ni mwepesi kuliko Mzambia huyo.

Chama tangu ametua Simba akitokea Power Dynamos ya kwao Zambia amekuwa akifananishwa kiuchezaji na Niyonzima ambaye msimu huu mambo ‘yamemkalia kushoto’ baada ya kukosa nafasi ya kucheza sana.

Niyonzima amesema yeye na Chama ni marafiki wakubwa na wamekuwa wakizungumza vizuri tofauti na wengi wanavyodhani yeye yuko juu zaidi ya Mzambia huyo kwa sababu mambo anayoyafanya uwanjani anafanya kwa utaratibu tofauti na yeye ambaye yuko fasta.

“Chama ni kiungo mzuri sana na anaujua mpira na mara nyingi tumekuwa tukizungumza vizuri kuhusiana na masuala ya uwanjani tofauti na watu wanavyoona kwamba eti sisi ni maadui.

“Hatufanani kiuchezaji kwa sababu yeye vile vitu anavyofanya uwanjani anafanya kwa uzito fulani hivi tofauti kabisa na mimi ambaye ninafanya hivyohivyo lakini kwa uharaka zaidi, hivyo hatuwezi kuwa sawa hata kidogo,” alisema Niyonzima.

2 COMMENTS:

  1. Chama zaidi na ametoa mchango wa maana uwanjani mpaka sasa tofauti na Niyonzima ambaye hata akicheza mipira anairudisha nyuma tu badala ya kupenya mbele. Umri umefika sasa Niyonzima aende kusomea ukocha afundishe timu ya Rwanda kama kocha msaidizi hii itakuwa na tija zaidi kwake.

    ReplyDelete
  2. Mmeishiwa habari au mnajisahau? Habari hii mliitoa siku ya Alhamisi, tena hvhv! na leo mnairudia tena!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic