Mshambuliaji wa timu ya Mbao FC, Said Khamis amesema kuwa kasi ya mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi inampa presha kwa kuwa amekuwa akipanda kadri siku zinavyokwenda.
Okwi mwenye mabao 7 kwenye ligi kuu alianza kwa kusuasua katika mechi za mwanzo na alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika mchezo wao dhidi ya African Lyon Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Khamis mwenye mabao 5, alisema kuwa amekuwa akifuatilia kasi ya washambuliaji wa ndani na nje ili kujifunza zaidi, amegundua namna Okwi ambavyo anapanda kwa kasi hasa kwenye ufungaji anapopata nafasi.
"Ukiangalia kwa sasa ana mabao 7 ambayo ameweza kuyafunga ila mechi zake za mwanzo alikuwa anatupia bao 1 baada ya mechi mbili kupita idadi ya mabao imeongezeka kwa kasi mpaka amefanikiwa kupiga 'hat-trick' hivyo kuna kitu cha kujifunza kwake.
"Malengo yangu ni kuweza kufunga mabao zaidi ya 20 msimu huu hilo linawezekana hasa kwa kuwa na mipango makini pamoja na kasi zaidi kama ilivyo kwa washambuliaji wengine, mashabiki waendelee kutupa sapoti kwa kuwa kazi bado inaendelea," alisema.








mtu mwenyewe magoli matano matatu klafunga ya penati halafu anajisifia acheze mpira kwanza
ReplyDelete