Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam, leo limeionyesha nyumba iliyotumika kumhifadhi Mfabiashara, Mohamed Dewji maarufu kama Mo alipotekwa.
Mo Dewji alitekwa na watu wasiojulikana Oktoba 11, afajiri akiwa anaingia mazoezini katika Hoteli ya Collesium jijini Dar es Salaam.
Juhudi za kumtafuta zilifanyika kwa takribani wiki mbili hadi watekaji hao walipomuachia.
Nyumba hiyo iliyo katika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam imeelezwa ilikodishwa kwa dola 1,500 na mtu mmoja anashikiliwa akihusishwa na watu hao wanaoelezwa kuwa ni raia wa Afrika Kusini.







0 COMMENTS:
Post a Comment