November 26, 2018


Ofisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa wanateswa na kauli ya Rais John Magufuli ya kuwataka waweze kushinda katika mashindano ya kimataifa hivyo hawatawaangusha watanzania.

Simba watacheza na Mbabane Swallows FC ya Swaziland Jumatano uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi ili waipe sapoti timu kwa vitendo.

"Magufuli alisema anahitaji tushinde na tulete ushindani hivyo tutahakikisha tunaitimiza kwa vitendo ahadi hiyo kwa kufanya kweli kwenye mchezo wetu wa kimataifa, mashabiki watupe sapoti.

"Mbabane ni timu nzuri, ni mabingwa wenzetu tunajua matarajio ya mashabiki wa Tanzania na mashabiki wa Simba, tumejipanga kuweza kupata matokeo," alisema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic