Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Yanga, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa kilichomrudisha Mwenyekiti wa Yanga, Yusuphu Manji ni matakwa ya wanachama wenyewe.
Mkuchika alisema kuwa Baraza la wadhamini liliitisha kikao na wanachama wa Yanga na kuwauliza ni wangapi wanamtambua Manji, wengi wao wakasema kwamba wanamtambua hata kama aliwaandikia barua ya kujiuzulu mwezi Mei 2017.
"Wanachama 4500 kwenye kikoa walisema kuwa wanamtaka Manji, tukamuandikia barua aweze kurejea kwa kuwa mimi ndiye niliyemuandikia barua, alipaswa kunijibu mimi mwenyewe niliyemuandikikia kama ambavyo ameniandikia.
"Barua inasema kwamba yupo tayari kurejea, ila atarudi rasmi kwenye kazi tarehe 15 januari 2019 kwa kuwa ni ushauri wa madaktari wake, hivyo kwa muda huu haendi kwenye ofisi zake za kampuni pamoja na shughuli za Yanga , Baraza la wadhamini limekubali kumkubali Mwenyekiti kwa kuwa barua tunayo na ni matakwa ya wanachama.

Uchaguzi January 13 yeye atarudi kuanza kazi January 15 changanya akili zako utajua kinachoendelea
ReplyDelete