November 11, 2018


Na George Mganga

Baadhi ya wanachama wa Yanga leo Jumapili jioni wamkusanyika kunako makao makuu ya klabu hiyo na kuanza kufanya fuji wakipinga kufanyika kwa uchaguzi wa kujaza nafasi za viongozi waliojiuzulu.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya baadhi ya viongozi wa Yanga kukubali kufanyika kwa uchaguzi huo ambao umepangwa kuwa tarehe 1 mwezi Januari 2019.


Moja ya viongozi ambaye amefanyiwa fujo ikiwa ni pamoja na kukoswakoswa ngumi ni Mjumbe wa kamati ya Utendaji Thobas Langalanga ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kaimu mwenyekiti wa klabu ya Yanga.


Wanachama hao wamesema hawataki kusikia suala la uchaguzi wakieleza bado wanamtambua Yusuf Manji kuwa ni Mwenyekiti wa klabu.

Wakati huo kikao cha Kamati ya Utendaji na Baraza la Wadhamini bado kinaendelea kunako Makao Makuu ya klabu sanjari na Wanahabari.

2 COMMENTS:

  1. Kama mpenda soka na unaipenda Yanga..suala kupinga uchaguzi ni suala la kurudisha maendeleo nyuma. Unaenda kupinga uchaguzu upuuzi kabisa..tena bila aibu kabisa eti unapinga uchaguzi???aibu sana tena ni wale wasiojielewa kabisa. Hatutarajii kuona hilo suala. We Kama bado unamuhtaji nenda kamwambie aje achukue fomu. Nahc Hawa ndio wale wasiotaka na kupenda maendeleo kabisa

    ReplyDelete
  2. Acheni kutupangia Mwenyekiti. Manji ndio mwenyekiti.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic