November 24, 2018


Kipa wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Manyika Peter, amefunguka kuwa kipa Klaus Kindoki hana sifa ya kuidakia Yanga kwani ana uwezo mdogo.

Kindoki raia wa DR Congo juzi alifanya makosa yaliyosababisha Mwadui kupata bao la kusawazisha, wakati akijiandaa kudaka mpira uliopigwa na Charles Ilamfya ulimgonga kifuani na kumkuta Salim Aiyee akauingiza kambani.


Manyika amesema Kindoki ambaye mpaka sasa ameruhusu mabao manne katika mechi tatu alizodaka hakuonyesha uwezo mzuri huku mabao mengi aliyofungwa yakitokana na uwezo wake mdogo.


"Kindoki hana sifa ya kuchezea Yanga kwa sababu kiwango chake ni cha kawaida, Yanga waache tabia ya kuwaamini wachezaji kutoka nje kwa sababu yule Kindoki anaonekana ni mvivu wa mazoezi haiwezekani wenzake wacheze vizuri kuliko yeye wakati mwalimu ni mmoja," alisema.


3 COMMENTS:

  1. Mnamzungumzia manyika Jr au manyika baba?

    ReplyDelete
  2. Mnamzungumzia manyika Jr au manyika baba?

    ReplyDelete
  3. Mwandishi hapo umetuchanganya, umeanza habari na Manyika Baba na umemaliza habari na Manyika mtoto, na mwisho wa siku hakuna anayekuelewa unamzungumzia Mayika yupi, duh!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic