November 24, 2018






Wapinzani wa Simba, Mbabane Swallows kutoka Swaziland wamefanya mabadiliko katika benchi la ufundi.

Swallows wamemuajiri kocha mkongwe kutoka Malawi, Kinnah Phiri kutoka Malawi ambaye aliwahi kuifundisha Mbeya City ya Mbeya.
Meneja wa Swallows, Sandile Zwane amethibitisha kwamba kweli wamemuajiri Phiri ili kujiimarisha kwa ajili ya michuano ya kimataifa.


“Tumeamua kumuajiri Kinnah kwa mkataba wa muda mfupi katika kipindi hike zaidi tukilenga michuano ya kimataifa,” alisema Zwane.

Aliyekuwa kocha wa Swallows amesimamishwa na baadaye kuondolewa baada ya kuingia kwenye tuhuma ya kumshambulia kijana muokota mpira.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic