November 14, 2018


Kiungo aliyeachana na KMC hivi karibuni, Abdulhalim Humud, amesema kuwa kuna timu ambazo yupo naye kwenye mazungumzo kuelekea dirisha dogo ambazo ataibukia kuzitumikia.

Humud aliwahi kuchezea Simba na Azam kwa nyakati tofauti hivi karibuni alivunja mkataba na timu yake kutokana na utovu wa nidhamu.

"Nipo bize kwa sasa nafanya sana mazoezi ili kuweza kujiweka fiti, sitaki kukumbuka yaliyopita kikubwa nahitaji kuona nafanyaje siku zijazo.

"Nipo tayari kujiunga timu yoyote kwa kuwa nina uwezo na kuna timu ambazo nipo nazo kwenye mazungumzo," alisema.

Humud alikuwa miongoni mwa kikosi ambacho kiliipandisha timu ligi kuu baada ya kufunga bao la ushindi katika mchezo wao wa mwisho wa ligi daraja la kwanza dhidi ya JKT Mlale.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic