Miaka saba imekatika sasa Simba imerejea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na wanajua watacheza na Mbabane Swallows FC kutoka Swaziland baada ya ratiba kupangwa.
Simba walifanikiwa kufika hatua ya makundi ya michuano ya kimataifa mwaka 2003 baada ya hapo wakapotea kabla ya kutwaa ubingwa msimu uliopita.
Swallows kwao ni mara ya pili mfululizo kushiriki michuano hii ambapo msimu uliopita waliishia hatua ya makundi sasa wamerejea tena kwenye michuano hiyo.
Swallows sio timu ya kubeza hata kidogo kutokana na msimu uliopita kuchukua Ubingwa wa Ligi ya Swaziland ikiwa na pointi 56 baada ya mechi 26 wakashinda mechi 17 wakatoka sare nane na kupoteza moja huku msimu huu wakiwa kwenye moto wao kwani walishinda kwa mabao 3-0 mechi yao ya hivi karibuni.
Simba walichukua Ubingwa baada ya kucheza michezo 30 wakiwa na Pointi 69 kibindoni baada ya kutoa sare michezo 9 na kupoteza mchezo mmoja huku wakishinda michezo 20.
Timu hiyo ilianzishwa mwaka 1948 mjini Mbabane huku Simba ikianzishwa mwaka 1936 ambapo kwa sasa ina mchezaji kama Asante Kwasi ambaye alichezea timu hiyo huku kwa upande wa jirani yupo Papy Tshishimbi ambaye alichezea timu hiyo.
Kocha wa Mbabane ni mzawa anaitwa Thabo Vilakati huku kwa upande wa Simba wakiwa chini ya Patrick Aussems raia wa Ubelgiji.
0 COMMENTS:
Post a Comment