November 22, 2018

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema hana hofu na mchezo wake utakaochezwa leo dhidi ya Mwadui FC kwa kuwa anawaamini watapata matokeo.

Zahera amesema kuwa anapenda kucheza ugenini ili kupunguza presha kwa masahabiki na wachezaji.


"Ukiwa nyumbani unakuwa na presha ya mashabiki ambao wanataka matokeo, wachezaji nao hucheza kwa tahadhari, ila ugenini unakuwa huru kufanya kile ambacho unakihitaji kwa umakini.


"Tatizo la ubora wa viwanja hilo nimeligundua na ndio maana hata mazoezi huwa tunafanya kwenye viwanja vibovu, muda utaongea," alisema.


Yanga wanacheza leo na Mwadui FC uwanja wa Kambarage ikiwa ni mchezo wao wa kwanza nje ya Dar, baada ya kucheza 10 uwanja wa Taifa wakiwa wamejikusanyia pointi 26.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic