November 22, 2018


Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya kupeperusha bendera kimataifa katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya Norhen Dynamo ya Shelisheli.

Mchezo hupo unatarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 27 au 28 kwenye uwanja wa Chamazi na marudiana yatakuwa 4 au 5 katika visiwa vya Shelisheli.


"Tumebeba dhamana ya watanzania katika michuano hiyo kazi yetu kubwa ni kuweza kupata matokeo hilo ndilo jukumu ambalo nimewapa wachezaji wangu, wote wanalitambua hilo," alisema.


Mtibwa Sugar wanaingia kwenye michuano hiyo baada ya kukamilisha adhabu yao ambayo walipewa ya kutoa faini baada ya kushindwa kupeleka timu kwenye michuano hiyo nchini Afrika kusini kutokana na Ukata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic