November 21, 2018


Kocha  msaidizi wa timu ya Azam FC, Iddy Cheche amewapa tahadhari wachezaji wa Simba kuwa makini na viungo wa Mbabane Swallow FC ya Swaziland kwa kuwa wapo vizuri.

Mbabane watacheza na Simba Novemba 28 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 4 au 5.


"Tulicheza nao kwenye Ligi ya Mabingwa hao Mbabane 2007, sehemu ambayo ni hatari kwao ni kwenye viungo wanasumbua wakiwa uwanjani kwa kuweza kukaa na mpira mguuni hali inayowafanya wafanye mashambulizi muda mwingi.


"Ili Simba wafanikiwe katika hili ni lazima waingie uwanjani kwa tahadhari kubwa, timu hii ni nzuri haipaswi kubezwa hata kidogo kwenye ushindani," alisema.


Azam FC walishinda kwa bao 1-0 walipocheza nyumbani na Mbabane kisha wakapoteza kwa kufungwa bao 3-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa Swaziland.

3 COMMENTS:

  1. Peleka ujinga uko tahadhari gani wewe umemshindwa unaongea nn kama wanakaa na mpira inakuhusu nn ikiwezekana wakalale nao wakae na mpira sisi tufunge ulichezea tatu unajua na simba atafungwa tatu kaa utulize mavi yako this is simba uje uwaokote apo taifa na tunakupa tahadhari na ww ukija na azam yako taifa ujipange

    ReplyDelete
  2. Simba Sports Club ndio inaongoza kwa kuwa na wachezaji viungo wazuri Tanzania

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic