November 21, 2018



Nyota wa timu ya Yanga waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa Stars, nchini Lesotho, Kelvin Yondani na Beno Kakolanya wameshindwa kusafiri na kikosi cha timu Yanga kilichoenda Shinyanga kucheza na Mwadui FC ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Chanzo kimeeleza kuwa wachezaji hao wamegoma kwenda na wenzao kwa kisingizio cha uchovu na kwamba wanahitaji kukaa na familia zao ambazo hawakuwa nazo kwa zaidi ya muda wa wiki tatu walipokuwa kwenye kambi ya timu ya Taifa iliyokuwa Afrika Kusini.


"Yondani na Kakolanya  hawajasafiri na timu kwa kudai kuwa wana uchovu pia Pato Ngonyani na Papy Tshishimbi wameshindwa kwenda hivyo safu yao ya ulinzi imepungua kwani hata Abdallah Shaibu 'Ninja' yupo na timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23," kilieleza.


Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa hajui kilichowakuta Yondani na Kakolanya kiasi cha kushindwa kuondoka na wenzao kwa kuwa ameskia tu ila hana taarifa kamili.


Kocha Mkuu Mwinyi Zahera amesema kuwa amepokea ripoti ambayo inaonyesha kuna baadhi ya  wachezaji hawajajiunga na timu mkoani Shinyanga hivyo anaifanyia kazi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic