November 24, 2018


Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema anaogopa kufanya mazungumzo rasmi na mastaa wapya watatu anaowataka kwa vile anaogopa masharti yao na hana hata senti mfukoni.

Zahera ameeleza kwamba wachezaji hao wana masharti mengi ya uhamisho na aina ya mikataba yao inahitaji fedha ambazo kwa hali halisi Yanga haina.

Kocha huyo anataka winga kutoka Ghana pamoja na straika na kiungo kutoka DR Congo. Bosi huyo alisikitikia hali mbaya ya uchumi inayoendelea ndani ya Yanga ambayo imefanya mpaka wachezaji Kelvin Yondani na Beno Kakolanya kugoma kwenda Shinyanga kucheza na Mwadui FC wakishinikiza malipo yao.

“Kupata mchezaji mpya lazima ufanye uhamisho, lazima ukae nae mjadiliane mshahara wake atalipwaje na hata mkataba wake utakuwa wa aina gani,”alifafanua Zahera ingawa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaaya alizishangaa tuhuma hizo jana akidai kwamba hawajakaa na kocha tangu atoke kwenye timu ya Taifa.

“Siwezi kufanya mazungumzo kwavile sijaona kiongozi yoyote yule aliyeniambia hayo masharti ya usajili tutayafanya namna gani. 

Inaelezwa kwamba viongozi wa kamati ya usajili wa Yanga wanaendelea kusajili kimyakimya na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji aliwapa masharti kwamba wamvumilie mpaka sakata la uchaguzi lipite ndipo atakapotoa fungu la kusajili kwavile bado muda utakuwepo.

Yanga wamefanya mazungumzo na beki wa Rayon ya Rwanda, Abdul Rwatubyaye na kumwambia asubiri kidogo.

4 COMMENTS:

  1. Yanga lazima tukubali kufanya uchaguzi na kupata viongozi watakao isaidia timu. Kumtegemea manji ni kujidanganya na kurudisha nyuma maendeleo ya klabu yetu

    ReplyDelete
  2. Yanga lazima tukubali kufanya uchaguzi na kupata viongozi watakao isaidia timu. Kumtegemea manji ni kujidanganya na kurudisha nyuma maendeleo ya klabu yetu

    ReplyDelete
  3. Enter your comment...yanga ni taasisi kubwa ambayo yenyewe inaouwezo wa kujiendesha kujitangaza kwakua Ina brand kubwa hvyo viongozi tunaowachagua lazima wawewanauwezo kiakili kiushawishi kifedha na mipango mikakati ya mda mfupi na mda mrefu kuhusu club na si kutafuta maslai yake binafsi Bali maslai ya club kwanza hvyo hatutakiwi kuchagua viongozi kwa mihemko kipindi hiki lazima tutulize akili wanachama pia tusijigawae makundi Bali tuungane tuisapoti timu yetu kuivusha ktk kipindi hiki kigumu sana kwani yajayo yanafurahisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic