November 24, 2018


Licha kuonesha kiwango duni ambacho hakikuwafurahishwa wengi katika mechi ya ligi dhidi ya Mwadui FC, mashabiki na wanachama baadhi wa Yanga wameuomba uongozi wa klabu hiyo kumpa muda Klaus Kindoki.

Kindoki alicheza mechi hiyo akichukua nafasi ya Beno Kakolanya ambaye aligoma kusaifiri kuelekea Shinyanga kwa madai ya mshahara, alifungwa bao la kusawazishwa wakati Yanga ikiwa imetangulia, bao ambalo wengi waliamini ni la kizembe.

Mashabiki hao baadhi wametoa yao ya moyoni na kueleza kuwa hiyo ni sehemu ya mchezo pekee na inahitaji kipa huyo kupewa muda zaidi ili kuzoea ligi ya Tanzania namna ilivyo.

Katika mechi hiyo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo mabao yake yaliwekwa kimiani na Heritier Makambo pamoja na Mrisho Khalfan Ngassa.

Kwa sasa Yanga tayari imeshawasili mjini Kagera tayari kwa maandalizi dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo ambao utapigwa Uwanja wa Kaitaba kesho Jumapili.

2 COMMENTS:

  1. Huo ni upuuzi. Huwezi mpa muda kipa wa kimataifa analipwa pesa zetu anzidiwa hata na kipa kinda. Aende zake, huyo ni mcheza sebene Kongo Zahera anatuletea eti mchezaji. Atutolee sisi takataka hyo ikacheze sebene fm accademia

    ReplyDelete
  2. Huo ni upuuzi. Huwezi mpa muda kipa wa kimataifa analipwa pesa zetu anzidiwa hata na kipa kinda. Aende zake, huyo ni mcheza sebene Kongo Zahera anatuletea eti mchezaji. Atutolee sisi takataka hyo ikacheze sebene fm accademia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic