November 24, 2018

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa mipango yake kwa sasa ni kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Mbabane Swallows FC ya nchini Swaziland.

Aussems jana alishindwa kuvunja rekodi ya Matola wa Lipuli FC, baada ya kukubali sare ya kutofungana licha ya kutengeneza nafasi nyingi.


"Nawaheshimu wapinzani wetu Mbabane sio timu ya kubeza ni timu nzuri hivyo nasi pia tutakuwa makini kuweza kupata matokeo, kwa kuwa kila kitu kinawezekana kwenye mpira," alisema.


Mbabane Swallows FC waliwahi kucheza na timu ya Azam FC mwaka 2007 walipoteza mbele ya Azam mchezo wa nyumbani kwa bao 1 na waliwashinda kwenye mchezo wa marudio kwa kuwafunga bao 3-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic