November 26, 2018


Kuelekea katika mchezo wao wa jumatano dhidi ya Mbabane Swallow FC ya Swaziland wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba utakaochezwa uwanja wa taifa, Simba wameahidi makubwa kwa mashabiki.


Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye ni kipenzi cha mashabiki amesema maandalizi yapo vizuri kwa kuwa wamekuwa wakipewa mbinu mbalimbali ambazo zitawafanya waweze kupata matokeo katika mchezo huo.

"Tupo vizuri wachezaji wote na tunatambua kuwa kazi iliyo mbele yetu ni kubwa, tunaomba Mungu tuweze kupata matokeo kwa kuwa hayo ndio malengo yetu kuweza kushinda mchezo wetu wa kimataifa.


"Jumatano tutakuwa uwanjani, mashabiki wajitokeze kwa wingi maana wana umuhimu sana katika kufanikisha ushindi, watanzania kwa pamoja watupe sapoti katika mashindano haya ya kimataifa hatutawaagusha," alisema Mkude.


Mbabane FC wanatarajiwa kutua leo kwa ajili ya mchezo huo wakiwa chini ya kocha wao wa muda kutoka Malawi ambaye aliwahi kuinoa Mbeya City, Kinah Phiri.

6 COMMENTS:

  1. HAMJITAMBUI NYINYI WACHEZAJI WA SIMBA KILA SIKU BAHATI SIO YENU

    ReplyDelete
  2. Simba ni sawa na sufuri,yani sufuri jumlisha sufuri sawa na sufuri.hamna spirit of fighting mnashindwa na yanga wakiingia uwanjani wanapigania timu kama jeshi la Israeli sasa sijui lini simba itaeleweka,inachosha na inakatisha tamaa,ndiomana unaambiwa mpira sio majukwaani wala mdomoni.

    ReplyDelete
  3. Simba ni sawa na sufuri,yani sufuri jumlisha sufuri sawa na sufuri.hamna spirit of fighting mnashindwa na yanga wakiingia uwanjani wanapigania timu kama jeshi la Israeli sasa sijui lini simba itaeleweka,inachosha na inakatisha tamaa,ndiomana unaambiwa mpira sio majukwaani wala mdomoni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli ulioyasema.No sprit of fighting.

      Delete
    2. Acha zako ww unaongea yasiyo na maana pambana na Hali yako

      Delete
    3. Acha zako ww unaongea yasiyo na maana pambana na Hali yako

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic