November 26, 2018


Mshambuliaji wa timu ya Stand United, Alex Kitenge ambaye alikuwa ni mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga 'Hat-trick' kwa kumtungua golikipa Klaus Kindoki, amewaita viongozi wa Yanga ili aweze kujiunga nao katika usajili wa dirisha dogo.


Kitenge amesema kuwa aliongea na Mwinyi Zahera na akakubali uwezo wake hasa baada ya kufanikiwa kuwafunga Yanga, hivyo anaamini akiwa ndani ya Yanga atafanya makubwa zaidi ya alipo sasa.


"Unajua mchezo wa mpira wakati mwingine unategemea unacheza na nani na katika mazingira yapi, imani yangu ni kwamba nikipata nafasi Yanga nitafanya makubwa zaidi japo wengi wanadhani nilibahatisha ila uwezo ninao wa kutumikia timu kubwa kama Yanga," alisema.


Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Yanga, Hussen Nyika alisema kuwa hawasajili ilimramdi wanasajili bali wanafuata maelekezo ambayo yanatolewa na Kocha Mkuu Mwinyi Zahera.


"Hakuna usajili wa ilimradi tu ndani ya Yanga, tunafuata ripoti ya kocha kama atatuambia anahitaji mchezaji fulani sisi hatuna hiyana tunafanya mazungumzo naye kisha anakuwa ndani ya timu yetu," alisema Nyika.

1 COMMENTS:

  1. Kitenge wa kawaida xana xio professional abaki hko hko xtand

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic