Mambo yakikaa sawa huenda winga machachari wa timu ya Rayon Sports ambaye ni raia wa Burundi, Bonfils Caleb akatua Simba kwenye dirisha dogo litakalofunguliwa Novemba 15, akiwa ni mbadala wa Shiza Kichuya ambaye msimu huu hajaonesha makali yake.
Kiungo huyo anayeitumikia timu ya Rayon Sports ya Rwanda, akiwa ana mabao 4 mkononi mwake katika ligi ya nchini humo baada ya mechi tano kuchezwa kwa sasa ameanza maongezi na viongozi wa Simba ili aweze kuongeza nguvu ya kikosi hicho.
Caleb amesema kuwa amezungumza na mmoja wa kigogo wa Simba ili kuweza kutua Msimbazi na kukamilisha mambo mengi yanayohitajika hivyo kwa sasa kinachosubiriwa ni tiketi tu ili atue Dar.
"Ni kweli nimezungumza na wakubwa, Simba wameniambia wananihitaji, nami nimewaambia kile ambacho nahitaji, mambo mengi tumekubaliana hivyo nasubiri tu mkataba ili niweze kusaini," alisema.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba zinaeleza kwamba kocha Mkuu, Patrick Aussems aliagiza atafutiwe winga machachari ambaye atasababisha madhara kwa Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco.
Kutoka Spoti Xtra

SAFI SANA KAMA ATAKUWA MACHACHARI ZAID ILI ALETE MAFANIKIO ZAID KWENYE TIMU YETU PENDWA SIMBA SC
ReplyDelete