Azam FC wamewapa mbinu Simba ya kuweza kupenya kwenye hatua ya makundi katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland kwa kuwa ni timu yenye uwezo ikiwa ndani na nje ya Uwanja.
Azam FC walicheza na Mbabane ambayo imeanzishwa mwaka 1948 na ni msimu wao wa pili kushiriki kwa kuwa msimu uliopita waliishia kwenye hatua ya makundi hivyo sio timu ya kuichukulia poa.
Meneja wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa ili Simba waweze kupenya kwenye hatua hii ni lazima watumie vema uwanja wa nyumbani kwa kufunga mabao mengi zaidi.
"Nyumbani tulifanikiwa kuibuka na ushindi, mwaka juzi kwa kushinda bao 1-0, marudiano huko ilikuwa balaa tulipoteza kwa kupigwa bao 3-0 nyumbani kwao, walitutoa kwenye mashindano mapema tu hivyo wapo vizuri kiushindani si wa kuwabeza.
"Watumie vizuri Uwanja wa nyumbani kupata matokeo, wale jamaa ni watata sana wakiwa kwao hivyo nguvu kubwa ianzie nyumbani," alisema.
Simba wanatarajiwa kucheza na Mbabane Swallows katika uwanja wa nyumbani kati ya November 27 au 28 na mchezo wa marudiano utakuwa kati ya tarehe 4 au 5 nchini Swaziland.








This is simba subiri utaona,watakula nyingi sana Mbabane yaani wengi wenu hamtaamin kitakachotokea siku hiyo
ReplyDelete