November 6, 2018


Kikosi cha Ruvu Shooting kimeweka rekodi ya aina yake baada ya kuweza kuruhusu mabao 9 kwenye mechi mbili idadi ambayo ni ya ajabu na ya kwanza kwa timu zinazoshiriki ligi kuu msimu huu.

Ofisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amekuwa akisema kuwa bado ana imani na kikosi chake licha ya kipigo ambacho wanakipata kwa kuwa kufungwa kwao haimaanishi hawana uwezo.


Mchezo wa kwanza kuruhusu mabao mengi msimu huu kwa Ruvu Shooting ulikuwa dhidi ya Simba ambao walifungwa mabao 5-0 kisha wakafungwa mabao 4-0 mbele ya Mtibwa Sugar hali iliyofanya wakusanye jumla ya mabao 9 mfululizo ya kufungwa .


Ruvu Shooting ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 12 wakiwa wamekusanya pointi 13 na kufungwa mabao 18 mpaka sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic