Vitalis Mayanga ambaye ni mshambuliaji wa timu ya Ndanda FC, ameweka wazi kuwa anatamani kuichezea Yanga na akitua hapo ndoto yake itatimia.
Mayanga ambaye kwa sasa ana mabao 5 kwenye ligi kuu alionyesha kiwango kizuri walipocheza na Yanga na kufanikiwa kumpiga chenga golikipa Beno Kakolanya kisha akatoa pasi ya bao na kuisaidia timu yake kutoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa.
Baada ya mchezo huo kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alikiri kukubali uwezo wa mchezaji huyo na kumhitaji kwenye kikosi chake ili aweze kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.
"Natamani kucheza Yanga na hata niliposikia kocha wa Yanga ananihitaji nilifarijika sana kwa sababu ni moja ya ndoto zangu, lakini siwezi kusema kama uongozi wa Yanga umenifuata au bado, ila nipo tayari kwenda Yanga," alisema.
Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Yanga, Hussen Nyika alisema kuwa kamati inafanya kazi kwa umakini kwa kuzingatia ripoti ya mwalimu kwenye usajili ili kuweza kupata wachezaji makini watakaoisaidia timu kiushindani.
Kutoka Championi








Mnavyojua kusifiaga ujinga, kupiga pasi mpaka kipa nyie kwenu ndio sifa kubwa kabisa
ReplyDeleteAna lolote uyo mchezaji akachukue kilicho bakia yanga maana ndanda ni hoya hoya tuu timu itakayo ifunga yanga ijisifu inakiwango watu watashangaa timu inazidiwa kuproses mpira mpaka na hiefuu yanga ni kama man u anapata matokeo bila mpango
ReplyDeleteWanayanga nashauri tuache wala tusishabikie wala kushiriki kwenye usajili wa wachezaji kwa kigezo cha kuwa aliwahi kutufunga kwenye mechi tulizocheza nao.
ReplyDeleteTuombeani uchaguzi wenye tija kwa Klabu yetu wene maneno maneno tupa kule.