November 24, 2018


Uongozi wa timu ya Lipuli FC, umesema umefika hatua nzuri ya mazungumzo na uongozi wa Simba ili waweze kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wao Marcel Kaheza.


Kaheza alisajiliwa na Simba akitokea MajiMaji FC ambayo imeshuka daraja kwa dau la shilingi Milioni 30, amekuwa akikosa namba kwenye kikosi cha kwanza kutokana na upana wa kikosi.


Kocha wa Lipuli, Seleman Matola amesema mpaka sasa wameweza kufika hatua nzuri ya maelewano na uongozi wa Simba kuhusu mchezaji huyo.

"Tumefanikiwa kufuata taratibu zote na kuzikamilisha hivyo kwa asilimia tisini tuna uhakika wa kumpata mshambuliaji Kaheza ili aongeze nguvu kwenye safu ya ushambuliaji maana bado haijakaa sawa," alisema Matola.


Kwa upande wa Simba kupitia Mratibu Abas Gazza alisema suala la mchezaji kuondoka hawana hiyana kumtoa mchezaji kutokana na upana wa kikosi kilivyo.


"Kama mchezaji atakuwa tayari kuondoka na timu ikafuata taratibu sisi hatuna kinyongo kwani tunahitaji kila mmoja awe huru, kama mchezaji atakataa kuondoka ni maamuzi yake maana ana mkataba na Simba," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic