November 11, 2018


Na George Mganga

Straika mwenye balaa la aina yake anayekipiga katika timu ya Difaa El Jadidi ya Morocco, Mtanzania Simon Msuva, amesema malengo yake ni kucheza pamoja na Sadio Mane huko Liverpool.

Akizungumza na Radio EFM kupitia kipindi cha E Sports jana jioni, Msuva ameeleza ndoto zake ni hizo kutokana na namna anavyovutiwa mchezaji huyo kutoka Sengal.

Msuva amefunguka kuwa hata kalba hajafika huko Morocco aliwahi kuweka picha yake mtandaoni aliyoiunganisha akiwa na Mane kama mchezaji anayemkubali kwenye maisha ya soka.

"Ninachoamini katika maisha kuna ndoto, naimani ipo siku itaweza kucheza sambamba na Sadio Mane kwakuwa ni mchezaji ambaye ninamkubali.

"Si kucheza naye tu, bali pia natamani kuichezea klabu ambayo Mane anacheza nikimaanisha Liverpoo, Mungu yupo na nina imani nitafika" alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic