MWIGULU NCHEMBA: TUNA HALI MBAYA SINGIDA UNITED
Mfadhili na Mlezi Mkuu wa Singida United, Mwigulu Nchemba, ameibuka na kueleza tena kuwa timu yao ni kweli imeishiwa hivi sasa.
Nchemba amesema Singida United inapitia wakati mgumu hivi sasa na kupelekea kusababisha baadhi ya wachezaji kuanza kuondoka kuelekea sehemu nyingine.
Siku takribani 5 zilizopita jumla ya wachezaji 6 waliomba kuondoka kutokana na klabu hiyo kuwa katika hali mbaya kiuchumu jambo lililosababisha malimbikizo ya mishahara.
Nchemba amelielezea suala hilo kuwa ni kweli na akisema imechangiwa na kuondoka kwa baadhi ya wadhamini waliokuwa wakiipa nguvu Singida.
Ukiachana na wachezaji, miezi kadhaa iliyopita timu iliondokewa na baadhi ya viongozi waliokuwa kwenye benchi la ufundi kutokana na kushindwa kulipwa stahiki zao.








0 COMMENTS:
Post a Comment