November 24, 2018

Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar, umesema kuwa umewaita viongozi wa Simba na Yanga ili waweze kuwaunga mkono katika mashindano ya kimataifa.

Ofisa habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema  watacheza na washelisheli siku ya jumanne majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.


"Timu mbili Simba na Mtibwa zinawakilisha Taifa kimataifa hivyo ni jukumu letu watanzania kuungana na kuwa kitu kimoja.


"Nimewaalika ndugu zangu wa Simba, Yanga, na Ruvu Shooting na timu zote kwa pamoja tuungane kupeperusha bendera yetu, watanzania wote tushirikiane," alisema.


Mtibwa Sugar wanawakilisha taifa kwenye Michuano ya Kombe Shirikisho ambapo Jumanne wataanza kupeperusha bendera kwa kucheza na Northern Dynamo kutoka Shelisheli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic