Uongozi wa timu ya Azam FC umesema kuwa baada ya kupata matokeo dhidi ya Ruvu Shooting akili zao wanazipeleka kwenye mchezo wao dhidi ya Stand United.
Azam FC wamefanikiwa kucheza michezo 13 bila kupoteza wakitoa sare 3 na kushinda michezo 10, watacheza na Stand United Desemba 4 uwanja wa Chamazi.
Ofisa habari wa Azam FC Jaffari Maganga amesema kuwa kipaumbele cha timu yake ni kupata matoeo chanya yatakayowapa nafasi ya kutwaa ubingwa.
"Hesabu zetu ni kwa kila mchezo bila kujali tunacheza na nani, tuna kikosi bora, walimu wazuri hivyo tunachohitaji ni matokeo kwa ajili ya mchezo wetu ujao," alisema.
Azam FC wanapointi 33 wakiwa ni vinara baada ya kucheza michezo 13, Yanga wanafuata wakiwa na pointi 29 wamecheza michezo 12, Simba nafasi ya 3 wakiwa na pointi 27 baada ya kucheza michezo 12.

0 COMMENTS:
Post a Comment