November 26, 2018


Kikosi cha Mtibwa Sugar, kesho kitakuwa uwanjani kupeperusha bendera ya Taifa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Northern Dynamos ya Shelisheli utakaochezwa uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.


 Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema ana imani na kikosi chake licha ya kutokuwa na wachezaji wa kigeni kutokana na mafunzo ambayo amewapa.

"Wachezaji wanatambua kazi yao na wamepata mafunzo makini kwa kuwa maandalizi tuliyaanza mapema hatuna mashaka katika hilo licha ya kutokuwa na mchezaji wa kigeni.


"Uzoefu walionao utawasaidia kwa kuwa tumecheza michezo mingi ya Ligi Kuu pamoja na ile ya kirafiki hali inayonipa imani kwamba tutafanikiwa kuipeperusha vema bendera ya nchi, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," alisema.


Tanzania ina wakilishwa na timu mbili kimataifa ambapo kwenye kombe la Shirikisho ni Mtibwa na kwa upande wa kombe la Mabingwa la Afrika ni Simba ambao watacheza na Mbabane Swallows FC kutoka Swaziland siku ya Jumatano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic